Jinsi ya kutengeneza Android App
January 15, 2021*Mh Esther Mahawe Anguruma Hanang kuinadi ilani ya CCM na wagombea wake wote*
October 20, 2020Mbunge mstaafu wa Viti maalumu Mkoa wa Manyara Comred Esther Alexanda Mahawe ameendelea kichanja mbunga ndani ya viunga vya mkoa mzima wa Manyara na leo ametua wilayani Hanang Mkoa wa manyara na kumuombea kura za kishindo Dr Magufuli pamoja na kuwanadi wagombea wote akiwemo Mhandisi Hhayuma mgombea ubunge Hanang pamoja Ndugu Portagia Baynit Mgombea udiwani Kata ya Nangwa.
Aidha mh Mahawe ameendelea kuwakumbusha wananchi wa hanang juu ya maendeleo makubwa tuliyoyapata kwa chini ya Dr Magufuli kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita hivo kumpa kura za kishindo kwa miaka mingine ni ishara ya kutambua mchango mkubwa wa kiongozi huyu aliyejitoa muhanga kwa ajili ya Taifa letu.
Mh Mahawe kesho ataendelea na zoezi la kuinadi ilani yetu na wagombea wetu wa ccm ndani ya kata ya Wareta. Wote mnakariibishwa.
Mwl Carol Gismoy
Mkt kamati ya Uhamasishaji Uvccm Manyara.
Mgombea Ubunge Hanang akirejesha fomu
September 06, 2020Mgombea ubunge Jimbo la Hanang akirejesha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Hanang mapema leo.
Nenda Baba Nenda Fr Massay RIP
August 18, 2020Maalum kwa Viwawa jimbo la Mbulu
August 14, 2020Dhana ya mwl nyerere ya kujitoa Muhanga
August 14, 2020MATOKEO KURA ZA MAONI CCM HANANG MANYARA
July 31, 2020Kura za maoni ubunge Hanang tunakamilisha
July 22, 2020Carol Gisimoy Aomba ridhaa kwa wana CCM Ubunge Hanang Manyara
July 07, 2020Mimi Mwl Carol Gisimoy (28) kwa Heshima, unyenyekevu na ujasiri mkubwa ninaoupata kupitia *wafilipi 2:3* huku moyo wangu ukiwa umejaa furaha na shauku kubwa nikitamani kwa dhati kabisa kuiona Hanang Yetu inapata ustawi zaidi na zaidi hasa kwa kuendeleza matamanio, matakwa, na ndoto za wananchi wake ambao sehemu kubwa ni wakulima na wafugaji.
Baada ya kutafakari kwa kina na kwa dhamira safi huku nikiendelea kumsihi Mwenyezi Mungu ndipo niliposikia sauti ya Bwana akisema; Nimtume nani naye ni nani atakayekwenda kwaajili yetu? Ndipo niliposema, mimi hapa nitume mimi (Isaya 6:8).
Ninaomba kuutaarifu Umma wa wana HANANG na viunga vyake kwamba nitakua miungoni mwa watia nia ya Ubunge wa jimbo letu la Hanang kupitia chama changu cha Mapinduzi na endapo chama changu kitaona ninafaa kwa mujibu wa katiba, kanuni, taratibu na Tamaduni zetu tulizowekewa na waasisi wetu tangu kuasisiwa kwake.
Upendo na Mshikamano kwa kila mmoja wetu unahitajika sana hasa zama hizi za kuhitajika kwa kila mmoja wetu tunao uwezo MKUBWA wa kuwa sehemu ya mabadiliko tuyatakayo na kwa kuitazama ile Spirit ya Rais Magufuli na aina ya mtu wa kuendana nae.
Kwa pamoja tunaouwezo wa kusimama kwa IMANI na kwa kupaza ya sauti zetu tukauamuru hata mlima wetu Hanang ung'oke na ukajitose ziwa basutu na ukatutii ili mwisho wa siku historia njema iandikwe kwa vizazi na vizazi juu ya uthubutu wa kizazi chetu cha ulimwengu wa leo.
Ninajua kwamba "Nikijiamini ... Nitastawi kwa uaminifu, Kwa heshima, Pia nitakuwa juu kwa utakatifu wa majukumu, Pia sitakuwa chini ya ulinzi wa wale waaminifu na utendaji usio na ubinafsi, Bila Hayo siwezi kuishi.
Kuna mzunguko wa kushangaza katika maisha ya wanadamu. Kuna vizazi vingine mengi walipewa. Katika vizazi vingine hasa tulichopo sisi Watanzania mambo mengi yanatarajiwa tu. Kizazi hiki Cha kutarajia, Kinahitaji watu watakaojenga matumaini hasa yatakayoonekana
Ninayoheshima kubwa kumpongeza kwa dhati mwakilishi wa jimbo langu kwa kipindi cha miaka kadhaa sasa Tangu 1995 akiwa Mbunge wa Viti Maalum wakati huo mkoa wa Manyara ukiwa bado haujazaliwa na baadae mbunge wa jimbo langu kuanzia 2005 mpaka sasa Dkt Mary Michael Nagu.
Mama huyu ni alama nyingine kubwa na tunu kwa Hanang yetu ukiacha ile ya kuwa na waziri mkuu mstaafu Mh Sumaye.
Ninayasema haya kwasababu maandiko yanatuambia " Amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu nao washindanao watapata hukumu" (warumi 13:3).
Kupitia kwenu mmeendelea kufanyika Mbaraka kwa kila mmoja wetu na utambulisho pekee wa Wilaya yetu kila tulipokanyaga mbakiwe sana. Hekima, busara na utashi wenu zinahitajika sana hasa katika kipindi hiki ambapo umoja, upendo,mshikama
Wenye Weledi husema Katika Kuamua Unapofikia mwisho wa kamba yako, funga fundo ndani yake na ushikilie.
#HanangMpyaCCMMp
#FikraMpyaMaonoM
#2020KataaRushwa
#BungeLaWanaHana
Ndimi mjoli wenu
Mwl Carol Naftali Gismoy
Sauti ya wanyonge Hanang 2020.
0783100301.
*IPO SIRI KUBWA SANA KATIKA UNYENYEKEVU*
July 03, 2020WAFUATAO Wamehamia CCM leo
June 14, 2020Jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM wilayani Hanang chini ya katibu wake comred *Raphael Ole Ngoitek
June 13, 2020#HabariPicha. Jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM wilayani Hanang chini ya katibu wake comred *Raphael Ole Ngoitek* leo imefanikiwa kufanya ziara yake ya kutembelea mradi mkubwa wa shamba la jumuiya hiyo zaidi ya ekari 130 iliyopo tawi la *Ninawi* kata ya *Gehandu* mbali na kuwapongeza viongozi wa kata hiyo kwa usimamizi imara wa mali za jumuiya, katibu huyo ametumia fursa hiyo pia kuwakumbusha vijana wote wa Hanang na viunga vyake kujitokeza kwa wingi kuchagua na kuomba ridhaa ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu utaofanyika mapema mwaka huu kwani wakati huu ni wakati muhimu sana kwa vijana hasa ukizingatia dhamira ya Mh Rais wetu ni kuhakikisha tunawapata viongozi imara na madhubuti kwa manufaa ya chama chetu na Taifa kwa Ujumla.
Uvccm Dodoma wasimama na JPM
May 25, 2020"Tunakila Sababu Ya Kumshukuru MWENYEZIMUNGU Kutuepusha Na Janga La Corona , Ndani ya Taifa Letu Na Ndio Maana Sisi Kama Uvccm Mkoa Wa Kilimanjaro Leo Tumekutana Hapa Kwa Lengo, Nia Ya Kumshukuru Mungu na Kuendelea Atuepushe Na Janga Hili La Corona." Asia Hamlaga Katibu Uvccm M) Kilimanjaro.
#ref-menu











