Jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM wilayani Hanang chini ya katibu wake comred *Raphael Ole Ngoitek
#HabariPicha. Jumuiya ya umoja wa vijana wa CCM wilayani Hanang chini ya katibu wake comred *Raphael Ole Ngoitek* leo imefanikiwa kufanya ziara yake ya kutembelea mradi mkubwa wa shamba la jumuiya hiyo zaidi ya ekari 130 iliyopo tawi la *Ninawi* kata ya *Gehandu* mbali na kuwapongeza viongozi wa kata hiyo kwa usimamizi imara wa mali za jumuiya, katibu huyo ametumia fursa hiyo pia kuwakumbusha vijana wote wa Hanang na viunga vyake kujitokeza kwa wingi kuchagua na kuomba ridhaa ya kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu utaofanyika mapema mwaka huu kwani wakati huu ni wakati muhimu sana kwa vijana hasa ukizingatia dhamira ya Mh Rais wetu ni kuhakikisha tunawapata viongozi imara na madhubuti kwa manufaa ya chama chetu na Taifa kwa Ujumla.
Awali mwenyekiti wa Uvccm Kata ya Gehandu Comred *Samweli Bajuta* alikiri kwamba mradi huu wa shamba ulikua ekari 116 lakini baada ya uhakiki wa mali za chama zilipatikana ekari 136 na kukabidhiwa rasmi kwa Jumuiya ya Vijana kata ya Gehandu tofauti na ilivyokua awali ambapo jumuiya haikua mmiliki wa eneo hilo Asahte Mh Rais na mwenyekiti wa CCM Taifa Dr JPM.
Aidha katibu wa Uvccm Wilaya ya Hanang amekagua pia ujenzi wa jengo la ofisi ya tawi la ninawi unaondelea kufanyika ikiwa ni matokea mazuri ya usimamizi wa mradi huo.
#TukutaneKazini
#UvccmMpyaHanangMpya
#CCMmpyaTanzaniaMpya
Mwl Carol Gisimoy
Mkt Kamati ya Uhamasishaji, Michezo na Maafa Uvccm Manyara.
#ref-menu


0 comments