Kura za maoni ubunge Hanang tunakamilisha
Nitumie fursa hii kwanza kumshukuru sana Mungu ambae kwake kila mamlaka hutengenezeka. (Warumi 13.1)
Niwashukuruni nyote ambao tangu mwanzo wa mchakato huu mmeendelea kunitia moyo na kuniombea na hatimae kwa pamoja tukahitimisha hapo jana kwa amani na utulivu wa kiwango cha juu kabisa.
Nipende kuwashukuru sana viongozi wa chama changu walioweka utaratibu huu mzuri kabisa wa kumpata mgombea wetu kwa kupitia wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya. Hongereni sana viongozi na wajumbe wote.
Mchakato huu umekamilika hapo jana kwa wajumbe wa mkutano,mkuu wa ccm wilaya ya Hanang kumpendekeza mgombea mwenzetu Ndugu Gorge Bajuta kwa kura 252 miongoni mwa wagombea wengine kwenye vikao vinavyofuata vya uteuzi. Pongezi nyingi kwako comred. Wagombea waliofuata tatu bora ni
2. Mary Nagu 206. Na
3.Eng Samwel Hayuma 139
Niwashukuru sana wagombea wenzangu wote 38. Sasa kwa pamoja tumempata mgombea anaeitwa #CCMHanang2020 tukamtetee naa kumsemea kwa nguvu zetu zote na pale ambapo tumekwazana kwa namna yeyote ile wakati wa mchakato huu niombe tusameheane na tuanze upya kwa nguvu zaidi kwa manufaa ya chama chetu na jamii yetu yote ya wanaHanang.
Kwangu mimi nimejifunza mengi mengi mengi sana na nitaendelea kujifunza zaidi kupitia kwenu viongozi na wanachama wenzangu, binafsi sikutegemea kabisa kushika nafasi ya 7 kati ya 38 ni Mungu tu alijidhihirisha kwangu.
.
#Ndugu wagombea wenzangu nipende kuwajulisha kwamba nimeunda group la pamoja la watsup kwa wagombea wote 38 lengo likiwa ni kuendelea kutiana moyo na kumpa nguvu yule ambae chama chetu kitamuona anafaa zaidi kwa mujibu kwa kanuni, katiba na tamaduni zetu tuliojiwekea hapo baadae.
Ahsanteni sana na Mungu atubariki sote.
Mwl Carol Gisimoy
#hanangmpya2020
#ref-menu

0 comments