Swift

Carol Gisimoy Aomba ridhaa kwa wana CCM Ubunge Hanang Manyara




Mimi Mwl Carol Gisimoy (28) kwa Heshima, unyenyekevu na ujasiri mkubwa ninaoupata kupitia *wafilipi 2:3* huku moyo wangu ukiwa umejaa furaha na shauku kubwa nikitamani kwa dhati kabisa kuiona Hanang Yetu inapata ustawi zaidi na zaidi hasa kwa kuendeleza matamanio, matakwa, na ndoto za wananchi wake ambao sehemu kubwa ni wakulima na wafugaji.

Baada ya kutafakari kwa kina na kwa dhamira safi huku nikiendelea kumsihi Mwenyezi Mungu ndipo niliposikia sauti ya Bwana akisema; Nimtume nani naye ni nani atakayekwenda kwaajili yetu? Ndipo niliposema, mimi hapa nitume mimi (Isaya 6:8).

Ninaomba kuutaarifu Umma wa wana HANANG na viunga vyake kwamba nitakua miungoni mwa watia nia ya Ubunge wa jimbo letu la Hanang kupitia chama changu cha Mapinduzi na endapo chama changu kitaona ninafaa kwa mujibu wa katiba, kanuni, taratibu na Tamaduni zetu tulizowekewa na waasisi wetu tangu kuasisiwa kwake.

Upendo na Mshikamano kwa kila mmoja wetu unahitajika sana hasa zama hizi za kuhitajika kwa kila mmoja wetu tunao uwezo MKUBWA wa kuwa sehemu ya mabadiliko tuyatakayo na kwa kuitazama ile Spirit ya Rais Magufuli na aina ya mtu wa kuendana nae.

Kwa pamoja tunaouwezo wa kusimama kwa IMANI na kwa kupaza ya sauti zetu tukauamuru hata mlima wetu Hanang ung'oke na ukajitose ziwa basutu na ukatutii ili mwisho wa siku historia njema iandikwe kwa vizazi na vizazi juu ya uthubutu wa kizazi chetu cha ulimwengu wa leo.

Ninajua kwamba "Nikijiamini ... Nitastawi kwa uaminifu, Kwa heshima, Pia nitakuwa juu kwa utakatifu wa majukumu, Pia sitakuwa chini ya ulinzi wa wale waaminifu na utendaji usio na ubinafsi, Bila Hayo siwezi kuishi.

Kuna mzunguko wa kushangaza katika maisha ya wanadamu. Kuna vizazi vingine mengi walipewa. Katika vizazi vingine hasa tulichopo sisi Watanzania mambo mengi yanatarajiwa tu. Kizazi hiki Cha kutarajia, Kinahitaji watu watakaojenga matumaini hasa yatakayoonekana wazi machoni pa Watumainio.

Ninayoheshima kubwa kumpongeza kwa dhati mwakilishi wa jimbo langu kwa kipindi cha miaka kadhaa sasa Tangu 1995 akiwa Mbunge wa Viti Maalum wakati huo mkoa wa Manyara ukiwa bado haujazaliwa na baadae mbunge wa jimbo langu kuanzia 2005 mpaka sasa Dkt Mary Michael Nagu.

Mama huyu ni alama nyingine kubwa na tunu kwa Hanang yetu ukiacha ile ya kuwa na waziri mkuu mstaafu Mh Sumaye.

Ninayasema haya kwasababu maandiko yanatuambia " Amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu nao washindanao watapata hukumu" (warumi 13:3).
Kupitia kwenu mmeendelea kufanyika Mbaraka kwa kila mmoja wetu na utambulisho pekee wa Wilaya yetu kila tulipokanyaga mbakiwe sana. Hekima, busara na utashi wenu zinahitajika sana hasa katika kipindi hiki ambapo umoja, upendo,mshikamano vinahitajika kuliko kipindi kingine chochote.

Wenye Weledi husema Katika Kuamua Unapofikia mwisho wa kamba yako, funga fundo ndani yake na ushikilie.

#HanangMpyaCCMMpya
#FikraMpyaMaonoMapya
#2020KataaRushwaKataaKanga.
#BungeLaWanaHanangWote2020

Ndimi mjoli wenu
Mwl Carol Naftali Gismoy
Sauti ya wanyonge Hanang 2020.
0783100301.

You Might Also Like

0 comments