Swift

*IPO SIRI KUBWA SANA KATIKA UNYENYEKEVU*

*IPO SIRI KUBWA SANA KATIKA UNYENYEKEVU*




Mungu alimteua binti mdogo sana *Maria* kutokea katika familia ya kawaida kabisa ili awe mzazi wa Mwana wa Mungu, ikumbukwe kwamba kila tarehe 01.01. ya kila mwaka huwa tunasherekea sikukuu ya *Maria mama wa Mungu* 
Nini hasa tunajifunza hapa? Tunajifunza kwamba vyeo vya kidunia na umashuhuri kwa Mungu si kitu chochote.
Mungu alipoamua kumuinua binti huyu mdogo *Bikira Maria* hapa anataka kutuambia kwamba yeye anaweza kumuinua yeyote amtakaye na kwa wakati wowote. 
Huwa inasikitisha sana baadhi yetu hatuko tayari kufanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wenzetu waliopo mpaka *TUPEWE* nafasi zao za uongozi, kila mtu hutenda jema pale tu endapo jambo hilo litamtangaza yeye kuwa ndio aliyetenda na hii ni hatari kubwa sana ya kutokujishusha.
Ni maombi yangu kwa mwenyezi kupitia kwa Mama kwa Mkombozi wetu Yesu Kristu *Bikira Maria* somo na msimamizi wa Taifa letu la Tanzania na jimbo letu katoliki la Mbulu awe msaada wetu pekee wa kujishusha nyakati zote.
Pamoja na kwamba yeye alikua Mama wa Mungu Yesu mwokozi wetu, lakini mara baada ya Yesu kupaa mbinguni Mama Maria aliendelea kuwa chini ya uongozi wa Mitume akiwemo petro tena yuleyule aliyemkana na kumsaliti mwanae. ( nawaza ingekua kizazi hiki cha kulipizana visasi ingekuaje? Mwacheni Mungu aitwe Mungu). Mama huyu hakuwahi kudai heshima yeyote kwa kigezo cha kumzaa Mwana wa Mungu.
Katika ulimwengu wa leo unakuta mtoto baba yake ana cheo fulani serikali hata miondoko yake tu inabadilika mfano mtoto wa polisi jamii pale basutu mtaa wa warangi kandokando ya ziwa basutu ni tofauti kabisa na mtoto wa familia ya kawaida iliyopo kwenye mashamba ngano pale nafco sasa jiulize kwa huyu Mama ingekuaje?
Marehemu bilionea *Regilald Mengi* aliwahi kusema kuhusu unyenyekevu na naomba ninukuu
"Ni mtu mmoja tu katika dunia hii ana haki ya kutokuwa mnyenyekevu! Ni yule siku ambayo ataitwa mbele ya haki ataweza kujizika mwenyewe." 

Ndimi mtumishi wenu
Mwl Carol Gisimoy
Mkt wa Viwawa Jimbo la Mbulu.

You Might Also Like

0 comments