USHUHUDA WA KWELI WA MAISHA YA DADA Flora Bayo Episode: 10
SEHEMU YA KUMI
Anaandika...✍️✍️✍️
Kwa muda wote WA ujauzito nilikuwa na Dr wangu ambaye ni specialist .Akaniambia tarehe 10.9.2019 watanifanyia operation. But tarehe saba mwezi huo WA tisa uchungu ukanianza mdogo mdogo. Nikapelekwa hospital. Tarehe nane mwezi wa tisa katoto kakachachamaa. Dr akawaambia manesi waniandae kwenda theater kama si kosei ilikuwa kwenye saa tisa ya mchana. Nikaandaliwa vema. Madktari wakawa wananijenga kiakili kuwa usiogope opareshen. Basi nikapelekwa mdogo mdogo mpk chumba cha oparesheni .kilichoniogope sha kidogo madaktari waliniacha chumba cha mapokezi wao wakaingia chumba cha ndani kwa muda kidogo. Baada ya dk kadhaa wakatoka mmoja wao akaja kuniambia Flora hatutakufanyia oparesheni kwasbabu una upungufu wa damu una hb 7 niliogopa nikamuuliza sasa itakuaje?? Akasema itabidi uwaite ndugu zako waje watoe damu ndio tukufanyie oparesheni. Nikamwambia hakika sina ndugu WA kumwita Kwan huku ni mbali nauli ya haraka haraka mtu WA kijijini ataipata wapi jamani isitoshe ndugu zangu wote ni walevi. Mimi ni binti WA pekee kwetu na nina kaka wawanne. Akasema hospital haina namna nyingine wakanirudisha wodini. Wakatoa dripu, mpira wa mkojo dah nililia sana nawaza nipate wapi damu. Muda ukawa unasonga na uchungu unazidi nikimwita nesi anasema hana namna. Lakini nikijaribu kutafuta mawasiliano ya ndugu zangu siwapati hewani. Nikamuuliza Mungu nikasema ee Mungu sikufa siku ya ajali kweli leo nakuja kufia hapa?? Nikamwambia tafadhali nifanyie wema wako kwa mara nyingine usiniache Mungu. Nesi akapima mapigo ya mtoto yakaw mia na Sabini na nne akakimbia kwenda kumwita Dr. Dr alipofika akasema vip umewapata ndugu zako nikajibu kwa uchungu siyo rahisi Dr naomba mnisaidie akasema hatuna msaada jitahidi waje hata kama ni usiku tutakufanyia oparesheni. Wifi yangu analia mi nalia. Wifi yangu akanipa chakula nikala kidogo by saa kumi na moja ya jioni Kwan nilishakata tamaa ya oparesheni.
Kwa muda wote WA ujauzito nilikuwa na Dr wangu ambaye ni specialist .Akaniambia tarehe 10.9.2019 watanifanyia operation. But tarehe saba mwezi huo WA tisa uchungu ukanianza mdogo mdogo. Nikapelekwa hospital. Tarehe nane mwezi wa tisa katoto kakachachamaa. Dr akawaambia manesi waniandae kwenda theater kama si kosei ilikuwa kwenye saa tisa ya mchana. Nikaandaliwa vema. Madktari wakawa wananijenga kiakili kuwa usiogope opareshen. Basi nikapelekwa mdogo mdogo mpk chumba cha oparesheni .kilichoniogope
Dr akaja akawaambia manesi kwa hasira mwandaeni dk tano namhitaji theater. Chapu chapu kazi ya kuweka drip ikaanza mara mishipa inakosekana nalia tu mara mpira WA mkojo dah ilikuwa ni mateso yasiyoelezekana . Kwa hasira akaniambia Panda kitandani yaani kitanda cha kupelekwa theater nikamjibu siwezi Dr ni ndefu sana akasema huwezi kwasbabu gani we si mzima kabisa! Manesi wakasema Dr jaman kweli hafiki. Chapu chapu wakanibeba wakaniweka kitandani yule Dr kwa hasira akanivuta kwa spread ya ajabu mpk nesi moja ananikimbiza kwa nyuma ili anifunike vizuri mi nalia tu. Nikamwambia Dr alafu nimekula. Akasema umekula tena aah!! Hivo hivo hatuna namna. Tulipofika Theater alawaambia wenzake alafu amekula Madkatr wakasema sasa tutafanyaje?? Wakasema hivo tufanye tu.
Kwa hofu na uwoga nikawa natetemeka kuna sauti inasema leo utakufa si unaona madktr wote wamekukasirikia nikawa nalia tu. Wao wakajiandaa wakavaa nguo za oparesheni wakati wanajiandaa nikaikemeea ile sauti nikasema ewe sauti nyamaza mimi nitaishi kwa msaada WA Mungu. Nikaanza kuimba kimoyo moyo ule wimbo unaosema Roho yangu naikuimbie jinsi wewe ulivyomkuu. Nikaimbaa mpk wao wakawa wamenizunguka. Nikamuuliza yule Dr Wang kuwa nitalala kwa masaa mangap maana waliniambia watanipa ganzi ya kulala usingizi yaani ya full. Akajibu kwa hasira siyo kazi yangu hiyo. Akasema muulize huyu yaani mwenzake nikamuuliza yeye akanijibu kuwa usiogope ni masaa machache tu. Basi moja wao akaniuliza kuwa flora utasali??
Kwa tabasamu la mbali nikajibu ndio. Akasema basi anza. Taratibu nikaanza kusali kwa kusema, Ee Mungu wangu najua siku ya leo imekupendeza mimi nijifungue naomba ufanye kazi pamoja na hawa madaktr ee Mungu uliyenitoa katika ile ajali naomba unitoe na hapa, uhai wangu upo mikononi mwako. Ameen wakati namalizia Ameen ni Kama kausingizi ukanipitia. Mwisho nikajikuta ni kama nipo sehemu na watu lakini ni kama Wale watu wapo busy busy. Mimi nilipoona vile nikaanza kuimba ule wimbo wangu wa Roho yanguuu........ ..
Kwa hofu na uwoga nikawa natetemeka kuna sauti inasema leo utakufa si unaona madktr wote wamekukasirikia
Kwa tabasamu la mbali nikajibu ndio. Akasema basi anza. Taratibu nikaanza kusali kwa kusema, Ee Mungu wangu najua siku ya leo imekupendeza mimi nijifungue naomba ufanye kazi pamoja na hawa madaktr ee Mungu uliyenitoa katika ile ajali naomba unitoe na hapa, uhai wangu upo mikononi mwako. Ameen wakati namalizia Ameen ni Kama kausingizi ukanipitia. Mwisho nikajikuta ni kama nipo sehemu na watu lakini ni kama Wale watu wapo busy busy. Mimi nilipoona vile nikaanza kuimba ule wimbo wangu wa Roho yanguuu........
Kumbe wakati naimba nilikuwa ICU na nilikuwa naimba kwa sauti. Baada ya muda nikafumbua macho nikawa naona kama giza Giza hivi. Nikawaona watu wawili wamekaa karibu yangu. Nikajiuliza kwani nipo wapi hapa? Nikapata jibu haraka haraka angali naongea kwa shida nikauliza yupo wapi mwanangu?? Wakasema yupo usiogope nikauliza tena ni wa kike au WA kiume wakasema ni wa kike. Nikasema ahsante Yesu. Nikawa najisikia vibaya nikasema Natakabkutapika wakaleta chombo nikatapika. Na kumbe nilikuwa natumia Oxsijen wakaondoa. Nikauliza yupo wapi dr wangu wakasema ngoja tukuitie wakamwita akauliza wow umeamka rafiki nikasema ndio ahsante maana yeye ndiye aliyemtoa mtt. Kwa ufupi nikapelekwa wodini. Wakamleta mwanangu kwa furaha nililia nikimshukuru Mungu.
Wodi ni walikuwa wanashangaa tu.
Glory to be God forever
Mwisho WA Simulizi nakushukuru Sana wewe uliyependa ushuhuda wangu Mungu akubariki Na Mungu akuinue akupitishe katika njia zote akikuongoza.
Now naitwa Ma Deborah. Adui zangu wote wamenyamazishwa Glory to God
Wodi ni walikuwa wanashangaa tu.
Glory to be God forever
Mwisho WA Simulizi nakushukuru Sana wewe uliyependa ushuhuda wangu Mungu akubariki Na Mungu akuinue akupitishe katika njia zote akikuongoza.
Now naitwa Ma Deborah. Adui zangu wote wamenyamazishwa
#ref-menu

0 comments