USHUHUDA WA KWELI WA MAISHA YA DADA Flora Bayo Episode: 7
SEHEMU YA SABA
Anaandika......✍️✍️✍️
SIMULIZI YA KWELI SEHEMU YA TANO!!
Ilipofika kwenye saa saba nikamwambia Mume wangu kwa machozi jaribu kutoa mguu nje ili utikise ili huku ndani watu wajue tupo hai. Mume wangu kwa huzuni akajibu siwezi kufanya chochote mke wangu. Nikamwambia usiogope mume wangu hatutakufa bali tutaishi na tutazaa watoto wazuri kwa utukufu wa Wa Mungu. Nikamwambia Sisi tutakuwa kioo kwa wengine usiogope tutatoka tu hapa. Baada ya dk kadhaa nikamwambia ngoja mimi nijaribu kama nitafanikiwa nikatoa mguu kwa kuunyoosha kwa nguvu nikautikisa huku nikiita Yesu, Yesu, Yesu tusaidie. Kuna mtu akaniona akasema kwa sauti jaman kimbieni njoeni muone kuna mtu anatikisa mguu. Wakaniambia tikisa nikatikisa wakasema mpk mara tatu tiksa mguu nikatikisa. Wakasema leteni shoka wakaanza kukata upande wa mume wangu wakafanikiwa kumtoa mume wangu. Wakati wanamvuta mume wangu akaniambia mke wangu usiogope nitasema upo hai wakutoe nami kwa kilio nikasema Sawa mume wangu. We nenda mi nitakuja. Basi walipomtoa tu nikamsikia mume wangu akisema jaman mwokoeni mke wangu yupo hai. Basi wakamkimbiza hospital. Wakaendelea kukata gari inavyosemekana wakamtoa mama moja ambaye ni jiran wa mume wangu na tayari alishafariki. Kabla hawajanitoa mimi nikasikia wakisema jaman mpini wa shoka umevunjika. Wakasema tutafanyaje sasa? Moja akajibu mkaifuate masqaroda. Kwa masikio yangu ninasikia pikipk inaondoka kwa speed kwenda kutafuta shoka. Wakati huo nimechoka mno nimeshameza damu za watu na za kwangu za kutosha. Nilipoona siwezi kuendelea kuomba nikamwambia Mungu umesema shukuruni kwa kila jambo hata kwa hili nakushukuru Sana. Nikarudi rudia hayo maombi kwa machozi huku nikiwa naongea kwa taabu sana. Baada ya muda pkpk ikarudi wakaanza kukata tena gari wakanipata wakanivuta wakanitoa. Huku nikisema ahsante Yesu watu walijua nimepaniki kumbe kweli nilikuwa na ufahamu muda wote. Wakanipelekea hospital ya Tumaini nikiwa najitambua kabisa. Na pia nawajua madktari walionihudumia wananihudumia huku nawaambia msiogope .

Madaktari wakahangaika Sana kuokoa maisha yangu. Wakaniwekea dripu ya damu kwenye shingo maana mishipa yote yalikuwa hayaonekani. Then wakanipeleka kwenye x ray wakagundua nyonga zimeachana. Kumbuka wakati huo wote nilikuwa sijui nani yupo hai nani kafariki. Nilipopelekwa wodini nikaanza kuwaulizia moja baada ya mwingine. Lakini nilimkuta wifi yangu mmoja kati ya watatu. Nikaanza kuwaulizia Wale wa wili mmoja mmoja wakawa manesi wananijibu kuwa wapo wodi nyingine wkisema vile mi nasema ahsante Yesu. Nikamuulizia ma mkwe naye waksema yupo nikasema Ahsante Yesu kwa machozi kumbe wote ninaowaulizia walishafariki pale pale. Nikiwa sijui hili wala lile by saa kumi na moja hivi wodi imejaa watu wakajua mi nimelala wakawa wananongo'na wanasema ma mkwe wake amefariki na wifi zake wawili nikapiga yowe kwa uchungu nikalia mno mno mno. Nikatulizwa pale wakati huo wkanifanyia rufaa wa haydom nikawa nalia tu naliano nilijutia kumshawishi mume wangu kufungia ndoa katesh. Nikawaza kuwa haya yasingetokea kiubinadamu nilijuta mno. Lakini mwisho nikaona nikubaliane na hali halisi. Nikarudia pale pale kwa kumwimbia Mungu nakushukuru kwa kila jambo ila nipe nguvu ya kustahimili hili nipe nguvu ee Mungu peke yangu siwezi siwezi huku nikilia tu. Nikapelekwa Haydom kwa amblence huku nikiwa na dripu ya damu. Tulipofika Hospital nikaingizwa kwenye chumba cha daktari. Lakini cha ajabu daktari akawa anawahudumia wagonjwa wengine wa kawaida yaani wale waliofika hospital kwa miguu yao au nisema hawapo serious zaidi ya masaaa sihudumiwi. Nikaanza kulia hata yule aliyenipeleka analia nikaanza kupiga kelele nikasema Yesu nisaidie angalia sihudumiwi lakini wewe nisaidie. Ndio yule Dr akasimama akawasitisha Wale ndio akaanza kuangalia fail langu. Oh! Akaniandikia vipimo hatimaye nikapelekwa wodini kuendelea na matibabu. Siku chache baadaye nikaona fb wamerusha picture zangu na kuandikwa kuwa huyu bibi harusi hatupo naye tena.
Walifariki watu saba na tulikuwa kumi na nne. Dereva na mwanaye walifia karibu yetu. Akafariki ma mkwe wangu na wifi zangu wawili na wifi mmoja alifariki na kijana wake aliyekuwa anasubiria matokea ya drs la saba. Na mama wa jirani. It is so sad.. Furaha yetu iligeuka kuwa msiba na vyakula vilivyoandaliwa vikawa vya msiba. It is so sad. It is impossible to explain.
Ulikuwa wakati mgumu sana kwangu kwa familia yangu na kwa mume wangu na familia yake. Mama yangu kwa uchungu alichoma nguo alizovaa siku ya send of na harusi. Alichanganyikiw a sana akawa anaongea tu ajali anaongea peke yake. Ila Mungu ni mwema alirudi ktk hali yake ya kawaida. Hadi Mungu anampumzisha alishaanza kusahau. R. I. p my beloved mom. Nakupenda mama najua upo sehemu ya kusubiria watakatifu wengine. We mbele yetu sisi tupo nyuma yako. I love you mom. My everything my comfort so mwaaa.
Okay ndivyo ilivyokua haikuwa rahisi kabisa kustahimili maumivu kwasbabu pia watu walinitabiria mabaya kila kukicha wanasema nimekufa lakini Mungu amenipigani now namshuhudia. Acha nimtangaze kabisa Yeye anaweza na anatosha.
Ulikuwa wakati mgumu sana kwangu kwa familia yangu na kwa mume wangu na familia yake. Mama yangu kwa uchungu alichoma nguo alizovaa siku ya send of na harusi. Alichanganyikiw
Okay ndivyo ilivyokua haikuwa rahisi kabisa kustahimili maumivu kwasbabu pia watu walinitabiria mabaya kila kukicha wanasema nimekufa lakini Mungu amenipigani now namshuhudia. Acha nimtangaze kabisa Yeye anaweza na anatosha.
Itaendelea..... ... SEHEMU YA NANE
#ref-menu

0 comments