*Mh Esther Mahawe Anguruma Hanang kuinadi ilani ya CCM na wagombea wake wote*
Mbunge mstaafu wa Viti maalumu Mkoa wa Manyara Comred Esther Alexanda Mahawe ameendelea kichanja mbunga ndani ya viunga vya mkoa mzima wa Manyara na leo ametua wilayani Hanang Mkoa wa manyara na kumuombea kura za kishindo Dr Magufuli pamoja na kuwanadi wagombea wote akiwemo Mhandisi Hhayuma mgombea ubunge Hanang pamoja Ndugu Portagia Baynit Mgombea udiwani Kata ya Nangwa.
Aidha mh Mahawe ameendelea kuwakumbusha wananchi wa hanang juu ya maendeleo makubwa tuliyoyapata kwa chini ya Dr Magufuli kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita hivo kumpa kura za kishindo kwa miaka mingine ni ishara ya kutambua mchango mkubwa wa kiongozi huyu aliyejitoa muhanga kwa ajili ya Taifa letu.
Mh Mahawe kesho ataendelea na zoezi la kuinadi ilani yetu na wagombea wetu wa ccm ndani ya kata ya Wareta. Wote mnakariibishwa.
Mwl Carol Gismoy
Mkt kamati ya Uhamasishaji Uvccm Manyara.
#ref-menu

0 comments