Swift

Dhana ya mwl nyerere ya kujitoa Muhanga


Dhana halisi ya kujitoa #Muhanga

Na Mwl Carol Gisimoy

Baba wa Taifa Hayati Mwl JK Nyerere aliwahi kusema nanukuu " Ili tuweze kufikia shabaha zetu kwa pamoja na kuifikia Tanzania tuitakayo ni lazima baadhi ya viongozi na wanachama wenzetu wakubali kujitoa MUHANGA kwajili ya wenzao hasa wale walio maskini, akaendelea akasema..  Sio mara zote chama chetu na serikali yetu imebahatika kuwapata viongozi wa aina hii waliokubali kujitoa muhanga kwaajili ya wananchi wenzao" hiyo ilikua Agost 16 1990.

Miaka 25 baadae katika nyakati chache ambazo nchi hubarikiwa tulipokea baraka ya kumpata Rais Dr John Pombe Magufuli ambae kwa hakika tangu mwanzo ameonyesha na anaendelea kuonyesha dhamira ya dhati ya kukubali kujitoa Muhanga kwaajili ya Wananchi anaowaongoza hasa Wananchi Masikini.  Hongera sana๐Ÿ‘๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
Ni muendelezo huohuo wa kumiminiwa baraka tunaendelea kujivunia viongozi wa aina yako ambao nao pia wameendelea kutembea kwenye nyayo zako. ๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

Nimebahatika kuisikiliza kwa makini sana na kuyarudiarudia  mazungumzo haya ya Mwenyekiti wa CCM Hanang Comred Mathew Darema akiwa anafungua kikao cha halmshauri kuu ya chama hicho wilayani hapo kilichoketi kwa lengo la kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Hanang Mh JJ Mkirikiti. Kwa hakika unaona kabisa dhamira ya dhati ya kukubali kujitoa muhanga kwaajili ya wengine bila kujali ukubwa wa vyeo vya wale wanaotumia muda wao mwingi kuifarakanisha, kuigawa na kuitenga Hanang yetu dhidi ya wawekezaji ambao ni faida kwa kila mmoja wetu.  Hongeraa sana comred huu ukiwa ndio wimbo kwenye vinywa vya kila mmoja wetu (Wanahanang)ni wazi kwamba nia yako na dhamira yako njema itafikiwa kwa kiwango cha Juu kabisa na kama ulivyosema mwenyewe Hanang yetu ITAPAA kwa kila nyanja na sio kutembea tena..!

Hongera kwa kuwapata viongozi mapacha wako Dc Comred Mkirikiti na DED Mh Kibasa mnaendana kwelikweli Mungu awabariki Sana kwa pamoja tunategemea kupata Hanang Mpya kupitia maamuzi yenu na viongozi wengine waliochini yenu๐Ÿ™๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
#MunguIbarikiHanang.
#MunguIbarikiTanzania.
#HanangIpaeZaidi.

Na Mwl Carol Gisimoy

You Might Also Like

0 comments