Swift

USHUHUDA WA KWELI WA MAISHA YA DADA FLORA BAYO Episode: 2


USHUHUDA WA KWELI WA MAISHA YA DADA
FLORA BAYO
SEHEMU YA PILI
Anaandika........✍️✍️✍️
Wacha tuendelee kidogo na ushuhuda. Mwaka 2003 nikapewa wheelchair so nikawa natembelea magongo na wheelchair. 2004 uti wa mgongo ukaniuma Sana,nikapelekwa hospital mbali mbali ila Hakuna ugonjwa hadi uti wa mgongo ukajikunja. Kwa maana hiyo basi hata urefu nilionao hata sasa ni wa darasa la nne baada ya mgongo kujikunja sikuendelea kurefuka. Maisha yangu yalijaa machungu, machozi, huzuni siku zote. Ila kilichonitia moyo nilikuwa napendwa sana na wenzangu. Nilikuwa na marafiki wengi sana. Siku ya jumapili tutunaamka mapema by saa kumi na moja na wenzangu wananisukuma na wheelchair mpk kanisani kuna saa wananibeba ili tu tuwahi ibada. Maisha yalisonga mbele nilikuwa mtoto niliyekuwa mgonjwa mara kwa mara hata mwalimu akiitwa kuwa kuna mgonjwa anajua tu ni flora. Haipiti wiki bila kulazwa hospital. Pamoja na hayo yote nilikuwa nasoma sana kwa bidii sana hata usiku wa manane naamka nasali then nasoma.. Ni.Nilikuwa nashika nafasi nzuri darasani.
Siku moja tulikuwa tumetoka kanisani mimi na wenzangu. Tukaona Tangazo la mkutano wa Injili. Imeandikwa Tangazo Tangazo kutakuwa na mkutano wa injili kuanzia tarehe 22/11/2005 hadi tarehe 24 ulikuwa mkutano wa siku tatu. Na mwisho wameandika tarajia muujiza wako. Nikawambia wenzangu siku ya mkutano nitapokea uponyaji na dunia Nzima itajua kuwa Mungu yupo. Siku tatu kabla ya mkutano nikafunga maombi nikamwambia Mungu nimesoma Biblia nimeona umeponya wengi naomba uniponye na mimi ili ulimwengu ukujue kuwa wewe upo. Nikamwambia ukiniponya nitakutumikia. Siku ya mkutano nikaenda na wenzangu kwenye mkutano tukakuta umati mkubwa sana wa watu hivyo basi hatukupata nafasi ya kupita mbele ili angalau niwe karibu na jukaa wakati wa maombezi. Basi tukaa nyuma sana wakati wa maombezi ukafika nikiwa kwenye kibaiskeli. Wenzangu wakaniambia itakuaje ili niombewe?? Maana tupo nyuma sana. Nikawajibu msiogope hapa hapa nilipo nitaponywa na Mungu kwa kuwa mkono wake si mfupi. Yule mtumishi akasema kama upo mbali weka mkono wako sehemu inayokuuma. Mimi nikaweka kwenye miguu yangu. Kimoyo moyo nikamwambia Mungu naomba uniponye katikati ya huu umati wa watu ili wewe ujidhihirishe kuwa unaweza. Yule mtumishi akaomba kama dk mbili hivi nikiwa nimefumba macho ghafla mwanga mkali kama radi ulipita katika mwacho yangu ikanilazimu nifumbue macho kwakuwa sijawahi kuona jambo kama lile. Nilipofumbua macho nikajihisi mwili wangu umechangamka, nikatikisa miguu nikaona yanasogezeka hakika niliruka juu nikapiga kelele nikisema. Nimepona!! Nimepona! Nimepona! Wenzangu walipiga kelele za shangwe na wengine waliokaa karibu yangu nao wakapiga kelele. Ikawa kelele kinyingi ikabidi yule mtumishi aulize kuwa kuna nini hapo?? Kwanini mnapiga kelele?? Watu wakajibu kwa sauti kuna mtu ameponywa. Basi wahuduma wakabeba baiskeli ile mimi nikaanza kutembea mdogo mdogo kuelekea jukwaani kwasbabu mtumishi aliniita mbele. Nikatoa ushuhuda mbele za watu wote nikiwa natokwa na machozi ya furaha..
Natoa ushuhuda huu ili wewe uliyekata tamaa yamkini kwasbabu ya ugonjwa au jaribu la aina yoyote uinuke kwa mara nyingine tena. Ujue kuwa jaribu unalopitia ni Mungu ndio ameliruhusu. Usimwache Mungu kwasbabu ya jaribu. Bali jaribu likufanye uwe rafiki wa Mungu.
Haijalishi adui atahangaika namna gani kusudi la Mungu halibadiliki kamwe.
Na Mungu atabaki kuwa Mungu.
Itaendelea SEHEMU YA TATU..........

You Might Also Like

0 comments