Swift

USHUHUDA WA KWELI KUHUSU MAISHA YA DADA FLORA BAYO Episode: 3


USHUHUDA WA KWELI KUHUSU MAISHA YA DADA
FLORA BAYO
SEHEMU YA TATU
Anaandika.........✍️✍️✍️
Mungu akanijalia kuhitimu elimu yangu ya kidato cha nne. Then nikajiunga na Chuo cha maendeleo ya jamii Mbeya. Then nikajiunga na Diploma ya maendeleo ya jamii kwa miaka miwili Iringa. Nikahitimu 2015. Mwaka 2016 nikajiunga na degree ya social work katika chuo kikuu huria. Open university of Tanzania. Nilikuwa nachumbiwa kama wasichana wengine. Ila nilikuwa sijapata dhamira ya kufunga ndoa kwa wakati ule na na pia sijapata amani ya kufunga ndoa na mtu yeyote kati ya waliokuwa wananichumbia. Watu walinisimanga kwa maneno mabaya hasa wanawake wakisema nani atamwoa yule na hali yake kwanza atabebaje mimba? Wengine wakanishauri nisiolewe kwasababu ya hali niliyonayo wakisema utawezaje kustahimili maisha ya ndoa na hali yako? Wengine wanasema ndoa ina mambo mengi. Wengine wakasema kama shida ni mtoto ni heri nizae bila ndoa. Wengine wakasena ukibeba mimba unaweza ukafa kwasababu ya hali ya Hali yako sasa unatoa uhai wako kisa mtoto? Wangapi hawana watoto?? Ila mimi nilikuwa nawajibu kwa ujasiri kuwa mimi nitaolewa Na nitazaa watoto wazuri kwakuwa Mungu aliyenitoa katika magongo na baiskeli bado anaishi. Maisha yakasonga mbele nikawa na mchumba ambaye nilikutana naye nilipoenda kufanya huduma ya Semina ya neno la Mungu kijijini kwao. Nikamtambulisha nyumbani kwetu kwa wazazi wangu. Mwaka 2016 ambapo tukapanga kuwa ndoa ingekuwa mwezi wa tisa. Mwaka huo 2016. Siku moja nikiwa na huduma kule mererani nakawa nampigia simu akawa hapatikani. Kwa siku tatu mfululizo akawa hapatikani. Nikafanikiwa kumpata rafiki yake nikamuuliza kuhusu mchumba wangu kutokupatikana.Akaniambia Shem naogopa kukueleza utaumia sana, nikamwambia please niambie ni heri niumie kwa ukweli kuliko nijifariji, akaniambia jamaa anatafuta namna ya kukuacha kwasbabu Kwao yaani wazazi wake na ndugu zake wamemwambia ukimwoa flora hatutakuja kwenye harusi wala kwako hatutakuja kwasababu unamwoaje mlemavu?? Ataweza kubeba mimba? Atazaaje?? Na je asipozaa umeoa.
Maisha yakendelea nikaogopa kuwaambia wazazi kinachoendelea. Kila wakiniuliza nawaambia mambo yako Sawa. Marafiki wakiniuliza nawaambia kwa mwaka huu tumesitisha mpk mwakani kuna mambo hayajakaa vizuri kumbe ni Siri ya moyo wangu naumia ndani kwa ndani.. Nilikonda hadi nguo zilikuwa zinadondoka. Kula siwezi wala kwenda kwenye huduma siwezi nimekuwa wa kujifungia tu ndani. Shida siyo kuachwa shida ni kumtambulisha mtu na pia vile watu walivyonisema vibaya hata nilipomtambulisha mchumba wakisema tuone kama atafunga ndoa. Mwisho nikamwambia mama yangu kuwa yule kijan ameniacha kwasababu ya moja mbili tatu. Mama kwa uchungu akaniambia usiogope mwanangu huyo siyo mpango wa Mungu. Aliyeandaliwa kwa ajili yako yupo. Ilikuwa mwaka 2016 nilipoachana na huyo jamaa. Siku moja nikakaa chini nikawaza kwa kina nikajiuliza hivi ni wachumba wangapi wananipenda? Na ni wangapi wameniomba uchumba? Na huyu tumekutana lini? Na kipindi cha nyuma kabla yake niliishije? Na yeye ndiye mwanaume tu kwenye hii dunia? Na nimeacha huduma nyingi kwasbabu ya huyu tu? Nikajiuliza maswali mengi nikajiona mimi ni mpumbavu tena mimi ni mjinga. Nikasema kuanzia leo naanza maisha mapya kabisa. Nikamtumia message nikamwambia kuanzia leo nimekusamehe bure wacha tuishi kama marafiki wa kawaida. Nikaanza maissha mapya ya kuendelea na huduma ya Injili. Siku moja nikaenda kufanya mkutano wa injili moshi ilikuwa mwezi wa kumi na moja 2016 nilipokuwa kwenye huduma nikamwambia Mungu mimi nakutangaza naomba ikiwa nakutumikia wewe Mungu wa kweli naomba mwaka 2017 iwe ndoa yangu. Ili adui zangu wanyamaze kimya. Niliporudi nyumbn nikatoa sadaka nikamwambia Mungu kwa sadaka hii nipe mtu sahihi uliyemwandaa. Lakini kumbuka siku nilipokaa chini na kujiuliza maswali mengi mwisho niliomba toba kwa machozi nikaomba Mungu anisamehe kwakuwa najilazimisha kwa jambo ambalo hajalipanga yeye.
Itaendeleaaaa.......

You Might Also Like

0 comments