Swift

USHUHUDA WA KWELI WA MAISHA YA DADA FLORA BAYO Episode: 4

USHUHUDA WA KWELI WA MAISHA YA DADA
FLORA BAYO
SEHEMU YA NNE
Anaandika......✍️✍️✍️
Maisha yakaendelea nikiwa mtu mwenye uchungu muda wote nalia tu. Afya yangu ilikuwa dhaifu kwasababu sili kwa raha. Kila watu wakiniuliza kuhusu harusi nawajibu kuwa kwa mwaka huu tumeahirisha ni mpk mwakani. Kumbe nimeachwa ni Siri yangu. Sikuwa naumia kwasababu nimeachwa niliumia kwasababu nimemtambulisha na watu wengi wakajua flora ataolewa muda si mrefu. Kwa ufupi niliogopa aibu. Nikiwa nimekaa kwa kwa miezi kadhaa kila nikiitwa kwenye huduma nawajibu ratiba imebana kumbe moyo hauna amani. Kuna siku nikakaa chini nikajitafakari nikajiuliza maswali mengi nikajiona mimi ni mpumbavu tena nimemkosea Mungu kwa kuwa yamkini nalazimisha jambo ambalo siyo mpango wa Mungu. Mwisho nikamtumia yule kaka yaani mchumba msg nikamwambia nimekusamehe bure nawe utashuhudia ndoa yangu na utawaona wanangu kwa macho yako. Nikamwambia sisi ni marafiki kuanzia leo uwe na amani. Nikapata neema ya kwenda kufanya mkutano wa Injili moshi sehemu moja wanaita kibosho road. Nikiwa kwenye huduma nikamwambia Mungu naomba unipe msaidizi wa kufanya naye kazi yako hii. Nikamwambia Naomba ikikupendeza mwakani yaani 2017 iwe ndoa yangu. Basi niliporudi kutoka moshi nikamtolea Mungu sadaka nikanwamwambia kwa sadaka hii naomba unipatie mtu sahihi na ndoa yangu iwe mwakani hiyo ilikuwa mwezi wa kumi na moja 2016.
Mwezi wa kumi na mbili kuna rafiki wa mchumba aliyeniacha tulikuwa tunawasiliana maongezi ya kawaida ila kumbuka siyo yule aliyenipa taarifa ya kuachwa. Tukaendelea kuwasiliana mpk mwezi wa pili 2017 ndipo alipofunguka kuwa anataka kunioa. Nami kwa hasira nikijua wale ni marafiki tena ni viongozi wa kanisa moja. Ambapo aliyeniacha ni katibu wa kanisa anayenichumbia ni katibu wa kwaya kwa maana hiyo kila mmoja anamwongoza mwenzake. Nikamwambia umetumwa unijaribu eee.. Nikamwambia ukiendelea na hilo swala lako hakika nitakata mawasiliano na wewe. Lakini yeye ananijibu kwa hekima ya ajabu mno. .Tukaanza mahusiano ambaye ndiye mume na baba wa mwanangu.
Ingawa changamoto ilikuwa Kama ya yule wa akiyeniacha ila yeye alisimamia katika Nia yake. Akaniambia nisisikilize ndugu zake wanasema nini bali nimsikilize yeye tu.
nami kwa shingo upande nikajipa moyo. Tukaendelea na mahusiano mpk siku ya harusi yetu ilipofika.
Itaendeleaa................

You Might Also Like

0 comments