Swift

SIMULIZI YA KWELI YA MAISHA YA DADA FLORA BAYO Episode: 5

SIMULIZI YA KWELI YA MAISHA YA DADA FLORA BAYO
SEHEMU YA TANO.
Anaandika........✍️✍️✍️
Tarehe 14/10/2017. Nikisema hii tarehe na mwezi najua kila mtu atasema Ni Nyerere day. Yes ni siku ya Baba wa Taifa. Ilikuwa siku njema sana kwangu mimi na mume wangu pamoja na ndugu zetu. Kwanza ilikuwa ni harusi ambayo haikuwa na kamati kila mtu ukimwomba anajitetea kivyake nikamwambia mume wangu ikiwa ni kusudi la Mungu basi atatutetea. Naye akaniambia usiogope hata kwa biskuti na soda tutafunga ndoa. Mipango ikaendelea kwetu wakajipanga kwa sherehe lakini upande wa mume wangu alikuwa mpweke nikamshauri kuwa asiogope mchango nitakaopata nitampatia na nikamwomba ndoa ifungiwe katesh kwasababu mimi nina marafiki wengi watakaoweza kunisupoti. Basi nikagawa kadi za michango Mungu alinipa kibali ya kupendwa. Basi mwisho na yeye amechanga changa kwa wengine tukawatafuta watu tukawakabidhi hela tulizopata wao wakazipangia bujeti. Siku ya harusi tulipomaliza kula mume wangu akaniambia tutaenda nyumbn kwao ambapo ni babati. Sehemu moja wanaita duru. Nikamwambia mume wangu sina amani ya kusafiri naomba sisi tubaki. Akaniambia mwombe wifi yako ambaye ndiye dada yake mkubwa na ndiye msimamizi wa msafara. Nikamwita wifi nikamwambia naomba sisi tubaki katesh akajibu haiwezekani lazima twende wote na gari inatusubiri alafu akaondoka.. Nikamwambia mume wangu kwakuwa imeshindikana wacha nikavue Shela alafu tutaenda ..Nikaenda kuvua Shela Kwa huzuni nikarudi nikapanda gari. Ambapo tulikuwa na noah na haisi. Noa imewapakia ndugu wote wa mume wangu pamoja na maharusi lakini haisi imewapakia wanakwaya na wengine. Safari ikaanza haisi ikawa mbele noa yetu nyuma.
Itaendelea............

You Might Also Like

0 comments