USHUHUDA WA KWELI WA MAISHA YA DADA Flora Bayo Episode: 6
NAAM,
NAJUA ULIKIWA UKINGOJA MUENDELEZO WA USHUHUDA WA DADA YANGU.
USHUHUDA WA KWELI WA MAISHA YA DADA Flora Bayo
SEHEMU YA SITA
Anaandika......
Tulianza safari yetu kwa kusali. Huku sauti taratibu ya kwaya ikiimba. Yaani yule dereva alikuwa ameweka flash yenye nyimbo za Injili. Mume wangu na mimi tulikuwa tumekaa mbele. Ambapo Alikaa dereva, mtoto wa dereva, mimi na mume wangu. Nyuma yetu yaani siti inayofuata amekaa ba mkwe na mke wake na mama wa jirani na kijana wa wifi yangu aliyehitimu darasa la saba. Na vitu vya nyuma walikuwa wamekaa wifi zangu watatu na wengine. Kwa ujumla gari ilikuwa imebeba watu kumi na nne. Wifi zangu walikuwa wananitania kwa furaha tukawa tunacheka sikujua kuwa ndio wananiaga maskini. Isipokuwa mama alikuwa mpole na mnyonge na mkimya. Na wifi yangu moja wapo kati ya hao watatu wakati tunapiga piga picha aliniambia wifi Njoo tupige picha huku nikikubusu. Kweli akanibusu tukapiga picha sikujua kuwa ndio mwisho wa kuonana. Oh ee Mungu nitie nguvu. Ambaye ndiye msimamizi wa msafara na ndiye niliyemwomba sisi tubaki akakataa. Tulipofika sehemu ambayo tunatakiwa tutoke lami tuingie rafu road I mean tupo kushoto inatakiwa tuingie kulia. Moyo wangu ulishtuka natamani hata nipae nipite haraka nikiwa katik hayo mawazo kufumba na kufumbua... Nikasikia paaaaa!!!!! Mimi nikajua nimebasti kichwa nikapoteza ufahamu. Katika ulimwengu Fulani ni kama gari letu linapinduka pinduka kumbe ndivyo ilivyo. Mwisho gari ikatua paaaaa!! Hapo hapo nikapata fahamu nilipoteza ufahamu kama kwa dakika tatu mbili hvi. Nilipopta ufahamu cha kwanza nikasema Yesu Yesu Yesu Tusaidie, tusaidie. Niliposema hayo maneno mume wangu ni ni kama mtu aliyetoka usingizini akauliza kuna nini?? Nikamwambia ni ajali tusali tusiangamie Mungu atuokoe. Wakati huo mimi ni kama mtu anayesujudu mkono wa kiume nimeuingiza kwenye stealing ya gari na wa kushoto nimeulalia. Mguu moja nimeshoosha na mwingine nimekunja. Na kichwa changu na cha mume wangu vipo karibu karibu nikitikisika yeye anaumia na yeye akitikisa kichwa chake mimi naumia.
Baada ya kama dakika kadhaa hivi nikasikia kunapikipik imepaki wakasema kuna ajali imetokea hapa. Kumbuka hiyo ilikuwa saa tatu za usiku na pia kumbuka haisi imeshatangulia mbele na Noah yetu IPO nyuma. Kama dk kadhaa hivi Ile haisi ikawa imerejea kwasababu kutoka sehemu tulilolipatia ajali mpk sehemu tulilokuwa tunakwenda ni kama dk saba mpk tano. Waliporejea ndio wakawapigia simu Wale wanakwaya waliopelekwa nyumbn. Watu wakaanza kujaa wakizungumza nje sisi tunasikia ila sisi tukiomba msaada hawatusikii. Niliingiwa na hofu moyo wangu uliogopa. Mno. Kuna wakati nawaza kuwa gari litalipuka lakini nikakumbuka ebr 10.38 inayosema Mwenye haki wangu ataishi kwa imani hapo hapo nikakataa hofu nikaanza kukiri maandiko inayosema sintakufa Bali nitaishi nami nitayasimulia matendo makuu ya Mungu. Maneno hayo yakazidi kunipa ujasiri nikakumbuka isaya 41.1 nakuendelea inasema upitapo katika mwali wa moto hautakuunguza wala upitapo katika maji. Maneno ya Mungu yakazidi kunipa ujasiri wa kumwomba Mungu. Nikamwambia Mungu naomba ukumbuke sadaka zangu na huduma yangu ukatuokoe kwa tendo jema moja tu unalolikumbuka niliyofanya kwenye madhabahu yako. Kwa uchungu nikamwambia Mungu je sadaka ya mume wangu niliyokutolea ndio imeishia hapa? Nikamwambia wewe umesema mkono wako siyo mfupi hata usiweze kuokoa naomba utuokoe na mtego huu. Muda ukasonga mbele uokoaje unaendelea ila wameshindwa kutoa noa katika kichwa cha semi. Kumbuka semi ilikuwa imelalia Noah yetu na huku tumekandamizwa na madirisha na Mlango umelock. Ingawa ilikuwa siku ya furaha mwanzoni ghafla iligeuka kuwa majonzi na kilio kwetu na kwa wengine. Ikafika saa nne bado hatujaokolewa ikafika saa tano bado ikafika saa sita bado oh Roho Mtakatifu alizidi kututia nguvu. Nikamwambia Mungu angalia hatuna hewa na harufu ya mafuta ya petrol imekua kali mno na mume wangu ananiambia pumzi inakata kata nikamtia moyo nikamwambia usiogope Mungu atatupatia hewa.......
Itaendeleaaaa..
#ref-menu

0 comments